Nishachoka

Kila chenye marefu na mapana huwaga hakikosi mwisho
Oh oh, mwisho
Yanini kurumbana kukicha bila suluhisho
Oh oh, ohuu

Wenda kisicho ridhiki
Hakiliki sa ya nini tutoane roho
Nimepungukiwa kipi
Mbona naishi sina ata jiba la roho

Na ule utwana wa mapenzi kushindana mi na wewe
Niliuvumilia na sijaona tamaa
Sio kama siwezi kupata alie zaidi ya wewe
Ila hii dunia na najichunga sanaa

Tena naandika huu wimbo
Usijpe moyo labda nakufikiria
Nataka iwe fimbo
Kwenye sura ya choyo ukome kunifatilia

Naandika huu wimbo
Usijipe moyo labda nakuwaza sana
Nataka iwe fimbo
Kwenye sura ya choyo ukome kunilili, eeh

Nishachoka, nishacho
Nishachoka wacha ukweli nikwambie

Yani kukicha vijembe (nishachoka)
Dharau maneno (nishachoka)
Ooh masimango (nishachoka)
(Wacha ukweli nikwambie)
Nimechoshwa nawe

Kila donda lina historia
Badala ya moto majivu
Mangapi niliyavumilia
Adi nikakonda kwa wivu

Kipato cha jasho langu
Ulikidharau na kukinyanyasa
Utu thamani yangu ukasahau kisa anasa
Angalau mimi nshakuzoea
Dharau mama yangu hajakukosea

Huwaga navuta taswira
Ule utumwa wa penzi lako
Mpaka najiona taira
Kuyahifadhi mabaya yako

Ukimjinga pedi
Unamatilapa nikapenda
Upepo kwenye begi
Au maji ndani ya tenga

Tena naandika huu wimbo
Usijpe moyo labda nakufikiria
Nataka iwe fimbo
Kwenye sura ya choyo ukome kunifatilia

Naandika huu wimbo
Usijipe moyo labda nakuwaza sana
Nataka iwe fimbo
Kwenye sura ya choyo ukome kunilili, eeh

Nishachoka (nimechoka na wewe)
Nishachoka (siwezi ooh)
Nishachoka wacha ukweli nikwambie (acha nikueleze)
Yani kukicha vijembe (nishachoka)
Dharau maneno (nishachoka)
Oooh masimango (nishachoka)
Wacha ukweli nikwambie
Nimechoshwa nawe

Canzoni più popolari di Harmonize

Altri artisti di Afrobeats