Matatizo

Haiye ah!!
(Wasafi records)
Olelelele

Alfajiri imefika
Anga inang'aa
Mvua inaanza katika
Ghafla tumbo la njaa
Naweka sauti kwa spika
Nipate umbea wa dar
Mara simu inaita
Jina la anko twaha
Akisema, mama yu hoi kitandani
Kama si wa leo wa kesho
Na kupona sizani
Upate japo neno la mwisho
Mi ndo mtoto wa pekee
Nyumbani wananitegemea
Mdogo wangu wa kike
Hali duni alishagaolewa
Tizama jasho langu la mnyonge
Kipato hakikidhi mahitaji
Napiga moyo konde
Yarabi mola ndo mpaji

Matatizo, matatizo
Yatakeisha lin
Matatizo
Kila siku mimi
Ewe mola
Matatizo yatakwisha lini
Japo likizo
Nifurahi na mimi

Mola aliniumba na subira
Imani pekee ngao yangu
Mbona nishasali sana
Ila mambo bado tafalan
Mama kanifunza kikabila
Nikonde sana haini yangu
Tena nijitume sana
Na vya watu nisivitamani
Hata mpenzi niliyenae
Najua siku atanikimbia
Itanitesa ye ndo nguzo
Zile ngoja kesho badae
Atazichoka kuzivumilia
Anakosa hata matunzo
Ona, nadaiwa kodi nilipopanga
Nashinda road nikihanda
Nishapiga hodi kwa waganga
Kwa kuhisi narogwa
Nikauza maji na karanga
Nikawa dobi kwa viwanda
Ila kote ziro ni majanga
Mtindo mmoja
Mi ndo mtoto wa pekee
Nyumbani wananitegemea
Mdogo wangu wa kike
Hali duni alishagaolewa
Tizama jasho langu la mnyonge
Kipato hakikidhi mahitaji
Napiga moyo konde
Yarabi mola ndo mpaji
Matatizo, matatizo
Yatakeisha lin
Matatizo
Kila siku mimi

Matatizo, matatizo
Yatakeisha lin
Japo likizo
Nifurahi na mimi

Matatizo, matatizo
Yatakeisha lin
Matatizo
Kila siku mimi

Matatizo, matatizo
Yatakeisha lin
Japo likizo
Nifurahi na mimi

Canzoni più popolari di Harmonize

Altri artisti di Afrobeats