Aiyola

Wasafi

Aiyoo aiyola iyee
Aiyola mama
Aiyoo aiyola iyee

Nilifundishwa na bibi kijijini jinsi ya kupenda
Na mwanamke hapigwi na ngumi ila upande wa kanga
Tena mapenzi sio league, nikakubali kushindwa
Mi sikufunzwa giraji, tushindane risasi kwa panga
Mbona nilikudhamini mengi nikakusevia, aahh
Sitosema hadharani wengi wakayasikia, aahh
Sio wakunipanda kichwani, hukumbuki tulipotokea
Na kunishusha thamani, kipi nilichokosea
Ingawa kidogo nilichopata, nikajinyima uridhike
Ila hukujali ukanikatili moyo
Majirani walinicheka uliponiforce nipikee
Ahhh sio siri ilinivunja moyoo
Kisirani, ugomvi bila chanzo
Ni ukweli uko moyoni sina budi nilivue pendo
Ingawa kishingo upande

Aiyoo aiyola iyee
Sitaforce unipende
Aiyoo aiyola iyee
Ila kishingo upande mama
Aiyoo aiyola iyee
Basi bora uende mama
Aiyoo aiyola iyee

Sitosema mapenzi basi nimeumbwa na moyo
Moyo wenye matamanio na unapenda pia
Ila nitaijuitia nafsi nilikufanya chaguo
Ah chaguo la moyo kumbe ulipita njia
Nilivyowanyima ndugu visiri nikakutunzia
Usijeleta vurugu akili ukaitibua
Najuta kujitia bubuu, sitaki vya kusikia
Kisa pendo unisurubu mengi nishayafumbia
Mbona nilikuthamini mengi nikakusevia, ahh
Sitosema hadharani wengi wakayasikia, ahh
Sio wakunipanda kichwani, hukumbuki tulipotokea
Na kunishusha thamani, kipi nilichokosea
Kisirani, ugomvi bila chanzo,
Ni ukweli upo moyoni sina budi nilivue pendo
Ingawa kishingo upande

Aiyoo aiyola iyee
Sitaforce unipende
Aiyoo aiyola iyee
Ila kishingo upande mama
Aiyoo aiyola iyee
Basi bora uende mama
Aiyoo aiyola iyee

Ingawa kishingo upande
Aiyoo aiyola iyee
Sitaforce unipende
Aiyoo aiyola iyee
Ila kishingo upande mama
Aiyoo aiyola iyee
Basi bora uende mama
Aiyoo aiyola iyee

Kishingo upande
Kishingo upande, aaahh
Na maximise-o, aaaah
Harmonize baby
Harmonize baby

Canzoni più popolari di Harmonize

Altri artisti di Afrobeats