Umebadilika

Bora nilale nje kuliko humu ndani mi sitoweza
Maelewano hakuna ukinikosea wataka kubembelezwa
Hivi humu ndani mume nan
Ukinikosea huombi samahani
Hivi kwan w n mke gani
Kazi kiburi tu na kisirani

Kwanza nimechoka sana
Na zako kelele mi nalala bwana
Maana unaongea sana
Kila siku huishi lawama

Ina maana ninanyoongea hayana mana
Haya ndo matatizo yako mama
Au mwenzangu umeshapata kabwana
Wenda ndio kanakuchanganya
Umebadilika sana aah
Tofauti na nyuma aah
Umebadilika sana aah
Tofauti na nyuma aah

Hivi we mwanaume unanini
Leo umeamka na mimi
Maneno maneno ya nini
Au unataka visa na mimi iiiii
Na nitaondoka kelele kelele nachoka
Usinione mi lofa nakuangalia tu

Mimi sipigi kelele
Nakurekebisha Uelewe kosa lako wewe
Unapaswa unisikilizeeeee
Mimi si wakula vibandani
Kama hela mi siachi hapa nyumbani
Hivi kwani we ni mke gani
Usiejua kunitunza mme ndani

Mbona yako mi siyaongei nayoyasikia hukooo
Au unaona hunikosehi badili mwendo wakoooo
Siku ngapi hujalala nyumbani unasingizia kazini
Waniacha na watoto nyumbani kumbe unalala jiraniiii
Anhaaa

Ukweli naujua mimi wala sio wewe
Hayo mambo kakwambia nani usiyasikilize
Kumbuka tulihapa kwa mananii utakuwa wangu tu
Na mambo unayoyafanya hayafanani nakwambia mume wangu
Maumivu ya Penzi hayawezi kupoa kama mwiba unavokuchoma
Siwezi kukuacha we ndo mboni yangu unaelifanya jicho kuona

Na nitaondoka kelele kelele nachoka
Usinione mi lofa nakuvumilia tu
Umebadilika sanaaaaa
Tofauti na nyumaaaaa
Umebadilika sanaaaaa
Tofauti na nyumaaaaa

Mi naondoka (usiondokee)
Nimechokaaaaa (usichokeeeeeee)
Mi naondoka (usiondokee)
We vumilia sitorudia

Mimi mi naondoka (usiondokee)
Nimechokaaaaa (usichokeeeeeee)
Mi naondoka (usiondokee)
We vumilia sitorudia

Canzoni più popolari di Bright

Altri artisti di Pop rock